Nilianza kwa dua Nikachua na hatua Ya kutembea kwa jua Kumbe mie sikujua Ningepigwa na mvua Nikiongea kwa jua... Haya mambo mwajua Huvutia ka' maua Ila ni maovu yanaua Yatakufanya kufua Kisha kifuani utatua Hata nguo utazivua Ila utabaki ukizua Uhasama ukiibua Na hapo hutatatua Hali yako ukishaijua Hilo kaa ukijua |Wayua| Ushauri kwa ushairi