Tega sikio nikusimulie yangu wewe Kishamba changu kimejilima chenyewe Vifaranga navyo vikachukuliwa na mwewe Nimebaki kujifuta machozi mwenyewe Na vipi kichwani sina hata nywele Ama ndio msimu wa kupata upele Usiotibika wa moyoni huu uwele Nimechoka hata sisongi mbele Nahisi nafsi yangu imegoma Moyoni moto nao wanichoma Inaposambaratika yangu boma Tabibu wangu yuko Oklahoma Atakuja niganga nifurahi Obama Inapunja hisia zangu hali hii kali Na si ati gharama ya maisha ni ghali Kwa kuwa nimejimudu kwa kila hali Ila kwa kuvunjwa, hapa mimi sina mali Pa kujisetiri hapanijali, ntarudi tu Somali' |Safari-ya-chozi| #pieces